Friday, January 23, 2015

SOMO LA "Communication Skills" LAZUA MTAFARUKU


Ikiwa imebakia takribani wiki moja kabla ya kuanza kwa mitihani ya mwisho wa muhula, somo la "communication skills" limeleta sura mpya kwa wanafunzi wa mwaka  wa kwanza wa shahada wa idara ya kompyuta...
Hapo awali ilikuwa ikifahamika kuwa somo hilo litatungiwa mitihani tofauti kutokana na kufundishwa na walimu tofauti, wanafunzi wa jengo ama idara ya kompyuta wao walikuwa wakifundishwa na mwalimu raia wa kigeni kutoka marekani ajulikanaye kwa jina la Belinda Nicholes huku wanafunzi wa idara nyingine pia wao walikuwa na walimu wao tofauti. Jambo ambalo limepingwa vikali sana mara baada ya walimu hao kukaa kikao cha takribani saa mbili kujadili swala hili na hatimaye kufikia uamuzi kuwa wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza wa masomo bila kujali ni wa idara ipi watafanya mtihani wa aina moja.

Tatizo si ufanyaji wa mitihani, ila tatizo kubwa ni kuwa walimu hao walikuwa wakifundisha mambo tofauti. Mpaka hivi sasa wanafunzi wapo katika sintofahamu kubwa sana juu ya mtihani huo.

1 comment:

  1. Best Casino Site in India (2021) | LuckyClub.live
    Our #1 Online Casino in luckyclub.live India - 100% Welcome Bonus up to Rs. 2,000 + 200 Free Spins ⚡ Sign up & get latest promotions.✏️ Deposit ₹2500+ Welcome Bonus.

    ReplyDelete