Friday, January 23, 2015

UJENZI WA ZAHANATI YA WANAFUNZI WAZIDI KUIMARIKA



Moja kati ya mambo makubwa ambayo Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar yameyafanya mwaka huu ni pamoja na ujenzi wa zahanati ya wanafunzi.
Kiukweli suala hili limeiweka SUZA katika muonekano tofauti zaidi...
Ni kwa kipindi kirefu sana suala hili limekuwa katika midomo ya wanafunzi kuhusu nini kitafanyika endapo mwanafunzi atapatwa na ugonjwa ghafla, ukizingatia chuo kipo mbali kidogo ya mji ambapo hospitali na zahanati nyingine zinapatikana.
Lakini katika kuliondosha hili uongozi wa chuo umeanza kufanyia marekebisho moja ya majengo yapatikanayo ndani ya chuo hicho ili liweze kutumika kama zahanati kwa ajili ya kuweza kuwapatia wanafunzi huduma za kwanza pamoja na matibabu madogo madogo.

Hongera sana SUZA!!!!!

huu ndio muonekano wa jengo la zahanati

No comments:

Post a Comment