Wednesday, January 21, 2015

WANAFUNZI SUZA WALIA NA HOSTELI

Licha ya jina kubwa lililojijengea, Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar kina tatizo la sehemu za kuishi wanafunzi (hosteli) ambapo chuo kama chuo hakijafanikiwa kujenga hosteli za wanafunzi...
Kutokana na hali hiyo wanafunzi watokao mbali na maeneo ya chuo huamua kupanga vyumba katika maeneo jirani na chuo hicho, hali hii pia inalalamikiwa kuwa wanafunzi hao hutumia gharama kubwa sana ukizingatia na hali duni ya maisha ya familia zao.
Hivyo uongozi wa chuo kupitia serikali ya mapinduzi ya zanzibar inaombwa kuangalia kwa makini suala hili.

1 comment: