Wednesday, January 21, 2015

UCHAFU WA MAZINGIRA WAWATESA WANAFUNZI WA KAMPASI YA NKRUMAH


Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar kampasi ya Nkrumah walalamika juu ya mazingira mabovu ya kampasi yao.
Mmoja wa wanafunzi amesikika akisema mazingira yao ni machafu sana yanayotokana na kutosafishwa kwa maeneo pamoja na kutopunguzwa kwa vichaka vilivyo jaa kila sehemu ya kampasi hiyo...
Hivyo wanafunzi hao wametoa wito kwa uongozi wa chuo kuwa wasiisahau sana kampasi yao kwani nao ni sehemu ya chuo hicho. Inasemekana kuwa kampasi ambayo imekuwa ikitunzwa sana ni kampasi ya Tunguu hivyo hali hii huwafanya wanafunzi wa kampasi ya Nkurumah kuona kuwa wao wametengwa.
Kwa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu umegundua ni kweli kuwa kampasi ya Nkurumah imesahaulika sana katika upande wa usafi, katika kukuhakikishia hilo tumekuwekea ushahidi wa picha unaoonyesha uhalisia wa mazingira ya Kampasi ya Nkurumah pamoja na Tunguu.

Angalia picha hizi za kampasi ya Nkurumah:







Pia angalia picha hizi za hali ya mazingira ilivyo katika kampasi ya Tunguu:






Nadhani hakuna haja ya kuongelea tena swala hili maana ushahidi umejionesha wenyewe.

No comments:

Post a Comment